MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Rose Ndauka amekanusha kuhusu madai kuwa amekuwa akiitisha usahili kwa wasanii Chipukizi na kuwachukulia fedha bila kuwashirikisha katika filamu zake.
Rose amekanusha shutuma hizo baada ya wasanii ambao waliwahi kufika katika ofisi za mwanadada huyo kushiriki katika usahili na kunyimwa nafasi.
�Jamani si rahisi kuchukua kila mtu anayeshiriki katika usahili inawezekana kweli akawa na sifa lakini wasanii wa aina hiyo wakawa wengi hapo linakuja suala la bahati ya mtu, hata wale wenye sifa majina yao yanahifadhiwa kampuni inapohitaji wasanii wengine wale ndio wanaopewa nafasi ya kwanza na si vinginevyo,� anasema Rose.
Siku za nyuma baadhi ya wasanii chipukizi walilalamika kuwa Rose amekuwa akifanya usahili kwa lengo la kujipatia fedha kwani mara nyingi baada ya usahili kufanyika wasanii ambao uwapanafasi ya kuigiza uwa ndugu zake na rafiki zake wa karibu na si walioshinda katika usaili, jambo lililomepingwa na Rose Ndauka.
0 comments:
Post a Comment